Lengo kuu la NEHE-STRAT ni kubadilisha kazi na vipaji vya wanamuziki na wabunifu wa kujitegemea (independent artists) kuwa chapa zenye ushawishi na zenye kuingiza kipato. Kampuni hiyo inalenga:
Kuwakutanisha wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa.
Kutoa mwongozo wa kisasa wa jinsi ya kutangaza kazi zao kupitia mifumo ya kidijitali ili kupata watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi (streams & views).